TAARIFA zilizotufikia hivi punde ni kwamba aliyekuwa mwenyekiti na mfadhili wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki dunia usiku wa jana huko Florida, Marekani.
Mtoto wa marehemu, Mehbub Manji, amethibitisha kwa Mwanaspoti kuwa Manji amefariki saa 6 usiku wa kuamkia leo.
Endelea kutembelea tovuti na mitandao ya kijamii ya Mwanaspoti kupata taarifa zaidi juu ya msiba huu mzito kwa wanamichezo hususan Wanayanga.