Aweso aanza kikao rasmi, afika kwenye ofisi ya RC DSM

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso leo terehe 01 July 2024 ameanza rasmi ziara ya kikazi katika mikoa ya huduma ya Maji inayotolewa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) akiwa na lengo la kufuatilia hali ya huduma ya Maji na kusikiliza changamoto za wananchi.

Waziri Aweso ameianza ziara hiyo kwa kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Mhe Albert Chalamila na kufika ofisi za Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Dar Es Salaam na kukutana na Mwenyekiti wa Mkoa Ndg. Abbas Mtemvu na Uongozi wa Chama Mkoa kwa ujumla.


Mheshimiwa Aweso katika ziara hiuo ameambatana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng Mwajuma Waziri.

Related Posts