Makundi ya Kinamama Mkoani Ruvuma yapongeza programa ya Imarisha Uchumi na Mama Samia

Katibu Mteandaji Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa katikati akifuatilia jambo kutoka kwa washiriki hawapo pichani wakati Baraza hili lilipoifikisha Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia IMASA Mkowani Ruvuma, kushoto ni kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw. Peres Magiri ambaye pia ni mkuu wa wilaya nyasa na kulia ni Mtaalamu wa Program ya IMASA na pia Katibu Tawala Msidizi Mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Elizabeth Mshote. Picha na Mwandishi wetu, Songea Ruvuma

Katibu Mteandaji Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa akiteta jambo na kaimu mkuu wa mkoa Ruvuma Bw. Peres Magiri ambaye ni mkuu wa wilaya ya nyasa wakati baraza hilo lilipoifikisha Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia IMASA Mkowani Ruvuma. Picha na Mwandishi wetu, Songea Ruvuma.

Wasanii wa ngoma ya lizombe wakisherehesha wakati Baraza la Uwezeshaji Kiuchumi (NEEC lilipoifikisha Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia IMASA Mkowani Ruvuma. Picha na Mwandishi wetu, Songea Ruvuma.

Na Mwandishi wetu, songea Ruvuma

MAKUNDI ya kinamama, Vijana na Makundi Maalumu Mkoani Ruvuma yameipongeza Serikali kupitia Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa kuwapelekea Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) kwa kuwapatia mafunzo ya biashara na ujasiriamali ambapo pia inalenga kuwapatia mikopo.

Kauli hiyo ilitolewa na wananchi wa Mkoa huo kwa nyakati tofauti kuwa wanapongeza hatua ya baraza hilo kuwapelekea programa ya IMASA Mkoani humo ambapo walipatiwa mafunzo ya biashara na ujasirimali na pia inalenga kuwapatia mikopo.

“Program ya IMASA imekuja kumkomboa mwanamama wa kipato cha chini pamoja na vijana na makundi maalumu,” walisikika wakisema, na wanaaimini baraza hilo linateleza kwa weledi program hiyo na makundi hayo yapo tayari kufanya biashara na ujasirimali.

Bi. Sada Hassan Mkazi wa Wilaya ya Mbinga alisema anajishughulisha na biashara ya urembo, ususi katika salon yake na kupitia IMASA amejifunza na anaenda kutumia mafunzo hayo kuboresha biashara yake hiyo.

“Nimejifunza namna ya kuongea na wateja, kutunza fedha katika akaunti ili iweze kuwa sehemu salama na kuwa na sifa ya kukopesheka,” na alisema anaenda kuwa balozi kwa wale ambao hawakupata fursa ya kufika katika mafunzo hayo.

Bi. Sophia Mapunda Mkazi wa Kata ya Ruanda Wilaya ya Mbinga alisema katika kata yao ya Ruanda wanajihusisha na kilimo, wanalima mahindi, maharage, nyanya, mbogamboga, vituguu, na mazao mbalimbali.

”Pamoja na kwamba nipo katika kilimo pia anamiliki kioski anauza bidha mbalimbali ambapo humletea kipato,” uwezeshaji utakaoletwa na program hiyo utasaidia kutunisha mtaji wake , alifafanua.

Pia aliiomba IMASA kuona kata yao inakinamama, vijana na makundi maalum ambao ni wachapakazi na wanahitaji uwezeshaji wajikwamue kivipato ili waweze kuendesha familia zao na kushiriki katika uchumi wa taifa.

Bi. Glory Maganga Mkazi wa Songea Mjini, alisema anapika chakula katika shughuli mbalimbali na anasema aliposikia IMASA inaingia katika mkoa wa Ruvuma alipata furaha na analipongeza baraza kwa kuwafikishia programa hiyo.

”Nimeipoke IMASA vizuri imetuletea uwezeshaji wa mafunzo na tutapata mikopo ambayo inalenga kutukwamua wanawake,” itatolewa mikopo kwa masharti nafuu kwa makundi haya na tunaamini tutapata, alisema kwa kujiamini.

Alisema baraza limewafundisha namna ya kujisajili na taarifa zao kwa sasa zipo mitandaoni kwa wale ambao hawakushiriki wataenda kuwasaidia kujaza taarifa zao katika mtandao nao waingine katika kanzidata.

Awali Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi (NEEC),Beng’i Issa alisema wafanyabiashara na wajasiriamali wajifunze namna ya kuongea na wateja ili waweze kufanya biashara kwa faida zaidi na wawafundishe wafanyakazi wao kuwaona wateja ni wafalme.

“Kutokuwa makini katika kuwahudumia wateja unafukuza wateja na mfanyabiashara ujue mteja anahitaji kitu gani,”. Na vilevile lazima mjue sheria za kodi kupitia Malaka ya Mapato TRA ili taifa lipate mapato yake, alisitiza, Bi. Beng’i.

Pia alisema makundi hayo yanahitajika kutumia mintandao kuingia katika mfumo wa Kieletronic wa manunuzi ambapo humo wanaweza kutajisajili na kupata taarifa za zabuni zinazotolewa na halmashauri kwa ajili ya kuomba zabuni

Alisema pia Songea mjini panahitaji kuwa na Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ambapo Halmashauri ya Mbinga tayari kuna kituo hapo wataweza kupata taariifa mbalimbali ikiwemo ya kuanzisha biashara, mikopo pamoja na bei ya mazao.

Related Posts