RC BABU AIPA HALMASHAURI YA SAME MWEZI MMOJA KUKUSANYA MILIONI 294.

NA WILLIUM PAUL, SAME.

MKUU wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu ameipa mwezi mmoja halmashauri ya wilaya ya Same kuhakikisha inakusanya fedha milioni 294 ambazo zilikuwa zimekopeshwa kwa vikundi vya wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.

Babu ametoa kauli hiyo wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo kujadili hoja tisa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30 mwaka 2023.

Babu alisema kuwa, fedha hizo zilitolewa na serikali kwa lengo la kuwainua uchumi na kuwakuzia mitaji hivyo ni lazima fedha hiyo iweze kurejeshwa ili kuwanufaisha watu wengine.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa aliipongeza halmashauri hiyo kwa kupata hati safi kwa miaka mitatu mfululizo pamoja na kupunguza hoja za Mkaguzi kutoka 40 hadi kufikia hoja 9.

Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni aliahidi kuendelea kuisimamia halmashauri hiyo ili kuendelea kupunguza hoja za Mkaguzi pamoja na kusimamia mikopo hiyo iweze kurejeshwa ikiwemo kuwachukulia hatua wale wote waliokopo.




Related Posts

en English sw Swahili