Simba yatambulisha chuma kipya kutoka Zambia

Simba imemtambulisha rasmi Joshua Mutale raia wa Zambia anayecheza nafasi ya kiungo mshambuliaji kuwa mchezaji wao kwa miaka mitatu.

Kiungo huyo aliyekuwa akikipiga Power Dynamos msimu wa 2023/2024 amefunga mabao matano na asisti tatu kwenye mechi 26 alizocheza.

Mutale mwenye miaka 22 anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani tena kwa ufanisi kwani anaweza kucheza kama winga ya kulia, kushoto na wakati mwingine anacheza nyuma ya mshambuliaji yaani namba 10.

Akiwa Power Dynamos msimu uliopita, Mutale amefunga mabao matano na kuisaidia kupatikana kwa mengine matatu katika michezo 26.

Related Posts