TUKUTANE SABASABA!! – MICHUZI BLOG

Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) inashiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 48 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam ili kuonesha huduma mbalimbali zinazotolewa na Bodi hiyo pamoja na utoaji wa elimu kwa wananchi waliofika kwenye Banda la Bodi hiyo lililo ndani ya jengo la Wizara ya Fedha.

Akizungumza na Michuzi Blog, Afisa Uhusiano na Mawasiliano Magreth Kageya amesema wanatoa huduma zote ikiwemo kutoa maelekezo ya jinsi ya kujisajili kwa ajili ya kufanya Mitihani, maelekezo kwa juu ya ulipaji wa ada mbalimbali na pia ametoa wito kwa wote wanaotaka kufanya usajili kwenye Bodi ya NBAA wanaweza kufika katika Banda lao.

Ameongeza kuwa kuanzia mwezi wa Septemba 2024 NBAA itaanzisha kozi mpya ya “Professional Diploma in Internal Auditing” (PDIA) ambayo itakuwa ni maalum kwa wakaguzi wa ndani

Amesema baadhi ya huduma zinazotolewa na NBAA katika kipindi hiki cha Sabasaba ni Usajili wa Wanafunzi ili kuweza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya chini (Accounting Technician) mpaka ile ya Taaluma (Profession) pamoja na usajili wa wanachama na makampuni ya Kihasibu na Kikaguzi.

Pia amesisitiza kuwa Bodi hiyo kwa sasa inatumia mifumo ya kidijitari kutoa huduma zake kwa kupitia tovuti yao.

Afisa kutoka NBAA, Estella Mgaya (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Anitah Rwechungura

kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi pamoja na vituo vya kusomea kwa ajili ya kufanya mitihani ya Bodi alipotembelea Banda na Bodi hiyo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 48 yanayoendelea kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.

Wafanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) wakiwa kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya 48 kwenye Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Es Salaam.

Related Posts