Ugonjwa wa kichaa cha mbwa unaweza kumpata binadamu kwa kuambukiza

Ugonjwa wa kichaa Cha mbwa umetajwa kuwa ni moja Kati ya magonjwa hatarishi Kwa wanyama hao pamoja na wafugaji kwani huambukiza Kwa kung’atwa na mnyama aliyeathirika na ugonjwa huo

Akizungumzia katika zoezi la utoaji wa chanjo ya kichaa Cha mbwa Marko Mabula mwanafunzi wa masomo ya Tiba za wanyama Chuo kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)kampasi kuu ya Morogoro amesema kuwa bila kutoa chanjo ya ugonjwa huu baadhi ya wanyama wamekuwa Wakiathirika Kwani ugonjwa huu huambukiza kutoka mnyama moja kwenda mnyama mwingine

Katika zoezi hilo zaidi ya mbwa 100 wamepatiwa chanjo hii kutoka katika hospital ya wanyama iliyopo Chuo kikuu Cha kilimo Cha Sokoine (SUA) ikiwa ni katika jitihada za Kupambana na ugonjwa huu pamoja na minyoo kwa wanyama

 

Pia Daktari wa magonjwa ya mifugo Mabula Mariko amewaomba wafugaji wote kuwapa chanjo wanyama hawa kwani zoezi hili ni endelevu

Akizungumzia faida za chanjo hiyo Daktari Philipo Otieno amesema kuwa Baada ya huduma hii kutolewa mfugaji anakuwa salama kwani ugonjwa huu huambukizwa maraa baada ya mbwa kumng’ata mnyama mwingine au mfugaji

Nao miongoni mwa wafugaji wa wanyama hawa ambao wamehudhuria katika zoezi hili wameridhishwa na huduma hii na wameiomba Taasisi kuhakikisha zoezi hili linakuwa endelevu mala kwa mala kwani mala baada ya chanjo hii mfugaji anakuwa huru na mnyama wake

Related Posts