Na Munir Shemweta
Jumla ya viwanja 4,150 vimemilikishwa katika mitaa 270 ya mkoa wa Dar es salaam kupitia programu ya ukwamuaji urasimishaji pamoja na klinik ya ardhi katika kipindi cha kuanzia januari hadi Machi 2024.
Aidha, programu hiyo imewezesha viwanja 55,034 kupangwa na vingine 6,824 kupimwa sambamba na elimu kutolewa kwa kamati za urasimishaji za mitaa 46 ambapo jumla ya viwanja 2,727 vinavyotakiwa kumilikishwa vimeibuliwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe. Timotheo Mzava ameishukuru serikali kwa kuwezesha ukwamuaji urasimishaji maeneo ya makazi holela kupitia Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki (LTIP) hasa ikizingatiwa zoezi hilo halikwenda vizuri siku za nyuma.
Katika ziara yake, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii ilipokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi za urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam, kuongea na kamati za urasimishaji za manispaa ya ilala pamoja na kugawa hati milki za ardhi kwa wananchi. Aidha, katika siku yake ya kwanza ya ziara yake jijini Dar es Salaam, kamati hiyo ilikagua miradi inayotekelezwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda akizungumza wakati wa mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika kwenye jimbo la Ukonga manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam tarehe 1 Julai 2024.Sehemu ya washiriki wa mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika mkutano uliofanyika Ukonga jijini Dar es Salaam Julai 1, 2024.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii wakiwa kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika mkutano uliofanyika katika jimbo la Ukonga jijini Dar es Salaam tarehe 1 Julai 2024.Mbunge wa viti Maalum mkoa wa Njombe Mhe. Neema Mgaya akimkabidhi mkazi wa Ukonga hati milki ya ardhi kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika Ukonga manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam Julai 1, 2024.Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe. Timotheo Mzava akimkabidhi mkazi wa ukonga hati milki ya ardhi wakati wa mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika jimbo la Ukonga tarehe 1 Julai 2024.Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Ardhi Maliasili na Utalii wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi wa jimbo la Ukonga waliokabidhiwa hati milki za ardhi kwenye mkutano wa kupokea taarifa ya utekelezaji zoezi la ukwamuaji kazi ya urasimishaji katika mkoa wa Dar es Salaam tarehe 1 Julai 2024. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI)