Kampuni ya Kobe Motor ya Japan imesema itaendelea kujitanua zaidi katika soko la Tanzania kutokana na kukua kwa mahitaji ya magari ya aina mbalimbali kwa ajili ya mtumizi binafsi na ya kibiashara. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).
Ikiwa ni moja kati ya makampuni makubwa ya Kijapani yanayouza magari yaliyotumika kutoka Japan sehemu mbalimbali duniani, Kobe Motor tayari imeshauza zaidi ya magari 150,000 hapa Tanzania na sasa inalenga kuongeza uuzaji wa magari zaidi hapa Tanzania na eneo zima la Afrika Mashariki.
Kwa mujibu wa Afisa Mtendaji Mkuu wa Kobe Motor, Umar Ali, Tanzania ni moja kati ya nchi 10 zinazoongoza kwa soko la magari kutoka Japan hivyo inaiona Tanzania kama soko muhimu.
“Lengo letu ni kuongeza uwepo wetu kwenye soko linalokuwa kwa kasi la Tanzania ambalo ni kitovu kwa ukanda huu wa Afrika Mashariki,” alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Akizungumzia kuhusu kampuni hiyo kuwa karibu na wateja wake, alisema Kobe Motor inashiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam na kuwataka watu kutembelea banda la kampuni hiyo kwa ajili ya kupata ofa pamoja na kujishindia gari kutoka Japan kupitia bahati nasibu itakayoendeshwa viwanjani hapo.
Katika hatua nyingine, Afisa mtendaji mkuu huyo alisema Kampuni ya Kobe Motor imezindua utaratibu wa wateja kulipa 35% ya thamani ya gari na kupewa gari la ndoto yao huku kiasi kilichobaki kikilipwa kwa kipindi cha miezi 12 au 24.
“Kampuni yetu inajivunia kuwa ya kwanza kuanzisha utaratibu huu utakaomwezesha mteja kupata gari la ndoto yake pasipo kulazimika kuwa na gharama zote za ununuzi wa gari,” alisema.
Aliongeza “katika dunia ya leo chombo cha uhakika cha usafiri ni muhimu na halikwepeki, kwa kutambua ukweli huu, Kobe Motor imekuja na aina mbli mbali ya magari ili na za gharama nafuu ili kumwezesha kila mtu kuwa na chombo cha uhakika cha usafiri,”
Alisema wafanyakazi wa Kobe Motor watakuwa katika viwanja vya Saba Saba kuwaelekeza wateja watakaokuwa wanaoagiza magari kwa mara ya kwanza taratibu za kufuata mpaka gari linapowafikia milangoni mwao.