Rapa Eminem kuja na albamu yake ‘The Death of Slim Shady (Coup De Grace)’

Rapa Eminem ametangaza tarehe ya kutolewa kwa albamu yake ijayo ya The Death of Slim Shady (Coup De Grace) kuwa Julai 12.

Rapa huyo alishiriki video ya promo kwenye mtandao wa kijamii ya albamu hiyo, ambapo mama anajifungua mtoto Mtoto mchanga, mwenye pembe zinazochipuka kutoka kwenye kichwa chake, akifungua macho yake meusi na kumpa mama tabasamu la kutisha.

Pia ameachia wimbo usiku wa kuamkia leo na umepewa jina la Tobey Maguire, aliomshirikisha Big Sean na Babytron

Hadi sasa, Eminem ametoa wimbo wa kwanza uitwao Houdini, akikumbuka wimbo wake wa 2002 Without Me.

 

Related Posts