Watoaji mikopo watakiwa kuwasomea masharti wateja wao kabla ya kuchukua Fedha

Meneja wa Mfuko wa Self Microfinance Mkoa wa Morogoro Moses Ntambi ambao uliopo chini ya wizara ya feda amezitaka asasi ndogo za fedha mkoa wa Morogoro kuweka wazi gharama, na masharti ya ukopeshaji wa fedha kwa wateja wao ili kuepuka malalamiko yanayojitokeza kwa sasa kwa watoa huduma hao.

Ntambi amesema hayo wakati wa mafunzo kwa wasimamizi na wakurugenzi wa asasi hizo ndogo za fedha yanayotolewa na Mfuko huo uliopo chini ya Wizara ya Fedha yenye jukumu la kutoa elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali na kutoa mikopo yenye riba nafuu

 

Ntambi amesema suala la asasi ndogo za kifedha kutoa mikopo kwa kufuata sheria,taratibu na kanuni zilizowekwa na Banki kuu ya Tanzania (BoT) ni la Lazima na kwamba.mfuko huo wa Self unatoa elimu ya fedha na utoaji wa mikopo nafuu kwa asasi hizo ambapo asasi 55 zilizosajiliwa Morogoro zimepatiwa mafunzo.

Akizungumzia suala la mikopo umiza maarufu kama kausha damu amesema wameendelea kutoa elimu zaidi kwa wananchi Ili kuwa na umeelewa wa kusima mshariti kabla ya kuokpa

Kwa upande wake Katibu wa Umoja wa wakopeshaji Tanzania wasiochukua Amana(TAMIU) Wambura Mirumbe alisema mafunzo hayo ni chachu ya kufanya kazi ya ukopeshaji kwa weledi,

Aidha Mirumbe alisema mwananchi anapotarajia kukopa ni vyema akajua taratibu, masharti na vigezo vyote vinavyohitajika pamoja na kujua mpoko anaouchukua ni kwa ajili ya lengo mahususi ili kuondokana na kuchukuliwa bidhaa ama dhamana yake bila sababu.

Naye Meneja Masoko na Uhamasishaji Mfuko wa Self Linda Mshana alisema baada ya kuona uwepo wa umbali baina ya taasisi zinazotoa mikopo kwa kukosa maarifa kamili kwa ajili ya kufanya kazi kikamilifu,ndipo mfuko ukaamua kuanza kutoa elimu hiyo ili kusaidia wananchi.

 

 

Related Posts