*Atoa kauli hii Banda la TIC Sabasaba
Na Mwandishi Wetu , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacinto Nyusi wametembelea Banda la Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwenye Maonesho ya Biashara ya 48 ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea kwenye viwanja vya Sabasaba.
Akiwa kwenye Banda la TIC, Rais Nyusi ameeleza utayari wa uwezeshaji wa usafirishaji wa bidhaa mbalimbali kwa njia ya Bahari kati ya Msumbiji na Tanzania hususan Tanzania visiwani (Zanzibar).
Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Gilead Teri ameitambulisha TIC namna inavyosaidia na kuwezesha uwekezaji nchini Tanzania, majukumu yake kwa ujumla, utoaji wa Huduma za Mahala pamoja kwa Wawekezaji, pamoja na vivutio vinavyotolewa kwa Wawekezaji.
Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam rasmi yamezinduliwa leo, Julai 3, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Jacknto Nyusi Nyusi akiambatana na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan