Balozi wa Tanzania Korea Kusini, Ndg. Togolani Edriss Mavura amethibitisha kupokea ugeni wa Wasanii wa Filamu Tanzania nchini humo na kufanya mazungumzo ya namna ya kuendeleza ushirikiano na Korea kusini ili kupata ujuzi na uzoefu zaidi katika kukuza Tasnia ya Filamu nchini Tanzania.
“Nimefanya mazungumzo na wasanii wa filamu wa Tanzania waliofika Ubalozini leo asubuhi. Wasanii wetu wako nchini Korea Kusini ikiwa ni maelekezo na matokeo ya ziara ya Mheshimiwa Rais Dkt. @SuluhuSamia nchini Korea Kusini ambapo pamoja na mambo mengine, alianzisha mazungumzo ya kupanua njanya za ushirikiano katika sekta ya filamu kati ya Tanzania na Korea Kusini.
Tanzania na Korea Kusini zinashirikiana katika sekta ya filamu kupitia MoU kati ya Jiji la Busan (Busan Global Citizenship Foundation) na Bodi ya Filamu Tanzania; na Mpango wa Mafunzo wa Miaka 3 wa Sekta ya Filamu (2024-2027) kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA).
Wasanii watatembelea taasisi za Filamu zilizoko jiji la Busan ikiwemo Busan Film Commission; Busan Film Studio; Busan Film Academy; Busan Cinema Corporation; na kuhudhuria Bucheon Fantastic Film Festival. Sekta ya Filamu ina mnyororo mkubwa wa thamani unaotoa ajira nyingi na kuzalisha mapato makubwa. Aidha, filamu ni kichocheo kikubwa kwa sekta ya utalii na diplomasia ya umma (public diplomacy).” ameandika Balozi Togolani Mavura
#KonceptTvUpdates