Baleke, Yanga jambo lao lipo hivi

HIZI huenda zikawa taarifa za kushtukiza kwa mashabiki wa soka nchini, kwamba baada ya Yanga kumbeba Clatous Chama kutoka Simba na Prince Dube aliyekuwa Azam, sasa inafanya mipango ya kumshusha kikosini, Jean Baleke aliyewahi kuwika na Wekundu wa Msimbazi hata miezi sita tu iliyopita.

Ndio, hivi unavyosoma Mwanaspoti ni kwamba kuna uwezekano wa asilimia 99 mshambuliaji huyo aliyeondoka katika dirisha dogo akiifungia Simba mabao manane akawa mali ya Yanga.

Taarifa lililonazo Mwanaspoti zinasema tayari nyota huyo raia wa DR Congo, keshamalizana na klabu hiyo, ingawa haijawa wazi kutokana na mfumo iliyoamua uongozi wa Yanga kwa sasa wa kufanya mambo kimyakimya.

Hata hivyo, chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Yanga kinasema kuwa, Yanga imemsainisha Baleke, lakini inafanya mchakato wa kumalizana na klabu ya TP Mazembe ambayo bado ina mkataba naye.
Baleke yupo jijini Dar es Salaam, anaonekana akifanya mazoezi sehemu mbalimbali, tangu arejee akitokea Libya ambako alikuwa anaichezea  Al-Ittihad mara alipoachana na Simba aliyokuwa akiichezea kwa mkopo akitokea kwa mabingwa wa soka wa DR Congo.

Kwa wanaokumbuka nyota huyo alifanya makala na Mwanaspoti na kuweka bayana kwamba, hana mpango wa kurejea tena Libya kutokana na hali ya usalama kuwa ndogo, kisha akatoa  wito kwa timu zinazohitaji huduma yake zizingatie taratibu za kuzungumza na TP Mazembe.

Chanzo hicho kilisema Baleke kasaini mwaka mmoja na endapo akifanya vizuri, ataongezewa mwingine.  
“Kasaini tayari, ishu inakuja ni kumalizana na TP Mazembe kwani bado ana mkaaba nao, hata timu ya  Al-Ittihad alikuwa anacheza kwa mkopo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Viongozi wanalishughulikia hilo, tayari wameanza mazungumzo na uongozi huo pia kufuatilia barua yake ya timu ambako alikuwa anacheza Al-Ittihad.”

Kabla ya taarifa za kusaini kwake Yanga, Simba iliwahi kurudi kuhitaji tena huduma yake, ambapo ilielezwa aliwahi kufuatwa na Juma Mgunda, lakini hawakufanikisha dili hilo.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, mabosi wa Yanga wameona Baleke ni mtu sahihi kumchukua kuliko Jonathan Sowah waliyekuwa wakimwinda tangu akiwa Medeama kabla ya kusajiliwa Al-Nasr Benghazi pia ya Libya ambaye alikuwa akihusishwa na klabu hiyo kama ilivyo kwa Manu Bola Labota aliyekuwa Singida BS (Ihefu).
 
TAKWIMU SIMBA
Alijiunga Simba usajili wa dirisha dogo la msimu 2022/23 alimaliza na mabao manane na msimu ulioisha alioachwa dirisha dogo alifunga mabao manane, hii ikiwa na mana kwa mwaka mmoja aliyoitumia timu hiyo nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 aliyewaji kukipiga FC Aigles RDC, Nejmerh SC na Mazembe.

Related Posts