Dodoma Jiji yafikia pazuri kwa Buswita, KMC yatua Uganda

DODOMA Jiji imeanza mazungumzo ya kupata saini ya kiungo wa Namungo, Pius Buswita baada ya kuridhishwa na uwezo wake.

Nyota huyo wa zamani wa Mbao, Yanga, Ruvu JKT na Polisi, msimu uliopita alionyesha kiwango bora na kufunga mabao saba na kuasisti moja katika Ligi Kuu Bara, inadaiwa hayupo katika mipango ya Namungo.

KLABU ya Pamba imefungua rasmi mazungumzo ya kupata uhamisho wa mshambuliaji wa TMA, Frank Ng’amba, kwa ajili ya msimu ujao.

Nyota huyo msimu uliopita alionyesha kiwango kizuri katika Ligi ya Championship ambapo alifunga mabao 15 kati 40 yaliyofungwa na timu nzima na kukiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya tano na pointi 54.        

MAAFANDE wa Tanzania Prisons iko hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wa aliyekuwa mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Meshack Abraham Mwamita.

Nyota huyo wa zamani wa Gwambina na Kagera Sugar, tayari amekubaliana maslahi binafsi na Prisons na muda wowote kuanzia sasa atatua Mbeya kukamilisha uhamisho huo na kusaini mkataba wa miaka miwili.

KLABU ya KMC iko hatua za mwisho za kukamilisha uhamisho wa kipa raia wa Burundi, Fabien Mutombora kutokea Vipers ya Uganda. Nyota huyo (27) amewahi kuichezea LLB Academic FC akikamilisha dili hilo, atakuwa wa pili raia wa Burundi kusajiliwa na KMC baada ya kumtambulisha kiungo mshambuliaji, Jean Nzeyimana kutoka Vital’O.

Related Posts