Shule ya Kamsamba, Tunduma day zapata wenyeviti wapya

WAJUMBE wa kamati ya bodi ya shule ya sekondari ya Kamsamba na shule ya kutwa ya  Tunduma zinazomilikiwa na jumuiya ya wazazi (CCM) mkoani Songwe wamewachagua wenyeviti watakaoongoza vikao vya shule hizo. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe…(endelea).

Uchaguzi huo umefanikiwa leo tarehe 4 Juni 2024 katika shule ya sekondari ya kutwa iliyopo halmashauri ya mji Tunduma wilayani Momba.

Katika uchaguzi huo mjumbe Ombeni Nanyaro amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa bodi wa shule ya Kamsamba na Neema Lwila amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa bodi Shule ya kutwa Tunduma.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo afisa elimu taaluma wilayani Momba aliyemuwakilisha afisa elimu mkoa, Michael Chawene amesema kupatikana kwa bodi hizo anaamini utatoa usimamizi mzuri wa shule na ufaulu.

Neema Lwila baada ya kuchaguliwa amesema kazi iliyopo ni kuhakikisha shule inaboreshwa na kuondoa ufaulu wa daraja la 4 na 3.

Naye Ombeni Nanyoro ni mwenyekiti mpya wa bodi shule ya Kamsamba amesema nafasi hiyo ni sehemu ya kutoa sadaka kwa watoto kwani mbali na kuweka mfumo wa maji safi na na kukarabati bweni atahakikisha anatoa motisha kwa wanafunzi na walimu ili kuongeza ufaulu wa alama A.

“Ili kufanikisha hili wazazi na walezi walete watoto wasome kwani shule hii ina mazingira salama na haina alama sifuri O wala 4. Kazi iliyopo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula na malazi safi na kufuatilia kwa ukaribu mienendo yao” amesema Nanyaro.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Taasisi ya Baraka Foundation Martin Mgalla amesema amepewa kandarasi ya kuiendesha shule hiyo na tayari ameanza kuyakarabati majengo chakavu kwa hatua ya mwanzo.

Aidha, Mwenyekiti jumuiya ya Wazazi wilayani Momba, Edward Silibwa amesema kabla ya uchaguzi wajumbe wa bodi za shule zote mbili wamepewa semina elekezi namna ya kuzisimamia shule hizo hivyo amaamini zitakuwa na ushindani katika ufaulu.

Related Posts