Wakala ya Barabara Tanzania ( TANROADS), imepokea tuzo maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Mheshimiwa Filipe Nyusi na Rais Mwenyeji wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tuzo hiyo imepokelewa na Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta leo tarehe 03 Julai 2024 katika ufunguzi wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Tuzo hizo maalum zimetolewa kwenye Taasisi tatu ikiwemo TANESCO, TANROADS na Taasisi ya Kichina ya Contro kwa kuthamini mchango wao mkubwa kwenye maonesho ya 48 ya Biashara Sabasaba.
#KonceptTvUpdates