Mwalimu wa VETA Kihonda William Munuo akizungumza na mteja kwenye Banda la VETA katika Maonesho ya Biashara Kimataifa ya 48 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
*Nikufuata madereva katika Ofisi zao bila kuathiri safari
Na Mwandishi WetuÂ
MWALIMU wa Magari Makubwa VETA Kihonda William Munuo amesema kuwa baada ya VETA Kihonda kuanzisha Program ya kufuata madereva katika Ofisi zao kumepunguza ajali kwa magari hayo.
Hayo ameyasema Munuo kwenye Maonesho ya Biashara Kimataifa ya 48 yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa katika kuwa Program hiyo imewafikia Madereva 5170 kati ya hao wanawake madereva 151.
Amesema kuwa kauli mbiu ya Maonesho Tanzania ni Mahala Sahihi kwa Uwekezaji hiyo inakwenda kuakisi kuwa madereva wanaosafirisha wanakuwa salama katika kutoa bdhaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Aidha amesema lengo la Chuo hicho ni kwenda kuwafikia madereva wote nchini katika Ofisi zao bila kuathiri safari za madereva za kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Munuo amesema kuwa madereva ni rasilimali muhimu katika sekta ya Uchukuzi ambao ndio dhamana ya bidhaa zote zinasafirishwa ndani na nje ya nchi.
Amesema kuwa katika Maonesho ya Sabasaba watu wafike ikiwemo madereva au wanaotaka kusomea fani hiyo kuweza kupata elimu ya kuendana na kazi hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa mafunzo hayo yamesaidia kwa wamiliki kutunzwa kwa magari yao na kuwa na uhakika wa safari kutokana na dereva kuwa sehemu ya kwanza kutambua gari.