Ziara ya Aweso yaimarisha huduma ya Maji Dar

Hali ya huduma ya maji kwa maeneo mbalimbali katika jiji la Dar es salaam na Pwani imeendelea kuimarika ikienda sambamba na ziara ya kikazi ya Waziri wa Maji, Mhe.Jumaa Aweso (Mb) iliyohitimishwa leo, Julai 4,2024 katika Wilaya za Kigamboni na Kinondoni.

Katika ziara hiyo Mhe. Aweso alitembelea maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mitambo ya maji, mantank ya kuhifadhi maji vinavyohudumia Wananchi wa Jiji la Dar es salaam na Mkoa wa Pwani na kukagua miundombinu ya usambazaji maji na kutoa maagizo ya kushughulikia changamoto za kihuduma kwa Wananchi.

Related Posts