Anayedai kulawitiwa na RC wa zamani Simiyu aibuka

Dar es Salaam. Mkazi wa Mwanza, Tumsime Mathias (21), anayedai kulawitiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda amefunguka, ikiwa ni mwezi mmoja baada ya tukio hilo.

Amesema anapitia magumu akilazimika kuhama maeneo tofauti kwa ajili ya usalama wake.

Tumsime ameeleza hayo leo Ijumaa Julai 5, 2024 alipozungumza na waandishi wa habari namna aliyokutana na Dk Nawanda.

Amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati kwa kuhakikisha mtuhumiwa anafikishwa mahakamani.

Amesema amelazimika kusitisha masomo kwa muda kutokana na hali halisi iliyojitokeza, akisisitiza suala hilo lipelekwe mahakamani ili haki itendeke kama yeye ana makosa basi aadhibiwe lakini kama hana basi mtuhumiwa achukuliwe hatua za kisheria.

Endelea kufuatilia Mwananchi…

Related Posts