Simba inadaiwa kuwa mbioni kukamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Awesu Awesu kutoka KMC kwa mkataba wa miaka miwili.
Mchezaji huyo anakaribia kujiunga na Simba baada ya kumaliza mkataba wake na KMC.
Awesu ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji na pia winga, ingawa kuna nyakati amewahi kutumika kama kiungo wa ulinzi.
Awesu anaachana na KMC baada ya kuitumikia kwa misimu mitatu tangu 2021 aliposajiliwa akitokea Azam FC.
Kiungo huyo pia amewahi kuzichezea Mwadui FC na Madini FC