Dk Biteko ataja wanachotaka wajasiriamali

Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk Doto Biteko amesema wajasiriamali lazima watengenezewe mazingira wezeshi katika eneo hilo ili wapambane na umasikini ambao kila mmoja anauchukia.

Dk Biteko amesema wanachotaka watu hao ni mazingira bora na rafiki hivyo jukumu la Serikali ni kuwatengenezea mazingira hayo.

Dk Biteko ametoa pongezi hizo leo Ijumaa Julai 5, 2024 wakati akizindua Kongamano la Wajasiriamali Wadogo, Wa chini na Wa kati, (MSMEs) lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City, Dar es Salaam.

“Serikali inafanya juhudi mbalimbali kama kutoa mikopo kwao mfano imetoa mikopo yenye thamani ya Sh2.3 bilioni, kutengeneza ajira, na hadi kufikia Machi, Serikali kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo imetoa mikopo na kuwekeza katika eneo la kilimo na mifugo.

Akitoa ushauri kwa kampuni mwandaaji ya MCL, Dk Biteko amesema ifanye namna ya kuwatangaza wale waliofanikiwa kupitia programu hizo ili kuleta chachu ya maendeleo yao.

Amesema kwa takwimu katika nchi zinazoendelea asimilia 90 ni mchango wa biashara hizo na asilimia 40 mchango kwa pato la taifa, asilimia 50 katika utoaji ajira ni wajibu kutengeneza mazingira wenzeshi katika eneo hilo lenye watu wengi.

Dk Biteko awapongeza MCL kuanzisha kongamano la wajasilimali

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati wa Tanzania, Dk Doto Biteko ameishukuru na kuipongeza Kampuni ya Mwananchi Communications Limitd (MCL) kuja na kongamano la wajasiriamali lenye lengo la kutatua changamoto zao hapa nchini.

“Niwapongeze MCL kwa kuendelea kuwa kinara katika kuandika habari na makala nzuri za kuuhabarisha umma pamoja na kuja na mpango huu ambao MCL inaangazia kusisimua biashara hapa nchini.”

Dk Biteko, ametoa pongezi hizo leo Ijumaa Julai 5, 2024 wakati akizindua Kongamano la Wajasiriamali wadogo, wa chini na wa kati, (MSMEs) lililoandaliwa na Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani city, Dar es Salaam.

“Hongereni sana kutuleta pamoja. Kitendo cha kukutana kujadili si sawa na kusemea nje, naamini katika mkutano huu utakuja na matokeo mazuri, kubadilishana ujuzi, sambamba na kutafuta soko,” amesema.

Amesema, kauli mbiu ya mwaka huu ya kongamano hilo ni wito wa kuchukua hatua kila mmoja katika kuhakikisha wajasiriamali wanapiga hatua.

Kongamano hilo lina lengo la kuboresha, kuendeleza ujuzi, na kukuza biashara zinazochipukia ndogo na kati linafanyika kwa mara ya pili ambapo kwa mwaka jana lilifanyika katika ukumbi wa Super Dome Masaki.

Related Posts