Kocha Fadlu Davids ametangazwa kuwa kocha mkuu wa Simba SC, baada ya kufikia makubaliano na uongozi wa klabu hiyo.
Kocha huyo raia wa Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 43 amesaini mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi cha Simba SC.
Kabla ya kujiunga na Simba SC, Fadlu alikuwa kocha Msaidizi wa mabingwa wa soka nchini Morocco Raja Club Athletic maarufu Raja Casablanca
Fadlu ambaye enzi zake alikuwa akicheza katika nafasi ya ushambuliaji anachukua nafasi ya Abdelhak Benchikha ambaye aliondoka wakati msimu wa 2023/24 ukiwa unaelekea ukingoni.
Mara nyingi Fadlu amekuwa muumini wa mfumo wa 4-2-3-1 ambao amekuwa akiutumia katika kila timu anayofundisha.