IAWP WAELEZA NAMNA WATAKAVYO DHBITI, MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO.

Na. Abel Paul, Abuja Nigeria.

Askari wakike Kutoka ukanda wa Afrika IAWP ambao wapo jijini Abuja Nchini Nigeria wameendelea na mafunzo yanamna ya kudhibiti uhalifu wa kimtandao na kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya Teknolojia pindi watakapo rudi katika mataifa yao.

Akiongea leo julai 04,2024 mara baada ya mafunzo hayo Naibu Kamishna wa uhamiaji kutoka Nchini Tanzania DCI Tatu Burhan Iddi amesema mafunzo hayo yamewapa mbinu yanamna bora ya kudhibiti uhalifu huo unapotokea.

DCI Tatu ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kutumia teknolojia hizo vyema ili kurahisisha kazi na huduma huku akisisitiza kuwa tayari wamejengewa uwezo wanamna watavyo wadhibiti wahalifu katika matumizi mabaya ya mitaandao.

Kwa upande wake Mrakibu Mwandamizi wa Polisi kutoka Tanzania SSP Georgina Matagi amebainisha kuwa wameona mifano mbalimbali ya kukabiliana na uhalifu wakimtandao huku akibainisha kuwa wanakwenda kuwafundisha askari wengine wanafanya kazi za kudhibiti uhalifu wa kimtandao nchini Tanzania.

Mrakibu msaidizi wa Polisi kutoka Nchini Nigeria ASP Kanem Inimfo amebainisha kuwa wamejifunza vitu vingi katika masuala ya uhalifu wa kimtandao huku akibainisha kuwa anakwenda kutoa elimu kwa jamii na kudhibiti uhalifu huo.

Vilevile Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka nchini Tanzania ASP Dkt Mwanaidi Lwena amesema kuwa licha ya kuwepo na mapambano ya udhibiti uhalifu huo nchini Tanzania amebainisha kuwa wamepata wasaha kubadilishana Mawazo na Nchi nyingine washiriki waliopo Abuja Nchini Nigeria namna ya bora kukabiliana na changamoto za uhalifu wa kimtandao.

Mkaguzi wa Polisi INSP Imani Pemba akaeleza namna walivyopata elimu ya kudhibiti Watoto wad ogo katika matumizi ya mitandao ya kijamii wakiwa na umri mdogo ambapo alibainisha kuwa kitendo hicho kimepelekea kuwepo na mmomonyoko wa maadili kwa Watoto na kuwa mafunzo hayo yanakwenda kuimarisha maadili kwa kundi hilo.

Related Posts