MADIWANI SAME WAMPONGEZA MAMA ANNE KILANGO KWA KUTETEA WANANCHI.
Na WILLIUM PAUL, Same.
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro wamempongeza mbunge wa Jimbo la Same mashariki Anne Kilango kwa kuwa mstari wa mbele kuwatumikia wananchi wake.
Mbunge huyo ambaye amekuwa akiwasilisha kero za wananchi wa Jimbo lake kila wakati kwenye Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania sambamba na kuzungumza na Mawaziri mbalimbali wa wizara tofauti kwa lengo la kutatua changamoto za wananchi wake.
Akizungumza kwenye kikao cha baraza la Madiwani kwa niaba ya madiwani wenzake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya Same, Yusto Mapande amesema katika vitu ambavyo Same mashariki wanajivunia ni pamoja na kuwa na mbunge ambaye siku zote amekuwa hazina kubwa kwa wananchi wake.
Mapande amesema katika kipindi cha muda mfupi Mama Anne Kilango amelisemea jimbo lake bungeni na amefanikiwa kupatia miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye Jimbo lake.
Amesema miongoni mwa miradi ambayo imetekelezwa na serikali kwa jitihada za mbunge huyo nipamoja na ujenzi wa Vituo 3 vya afya katika tarafa za Ndungu, Mamba Vunta na tarafa ya Gonja huku mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ukitarajiwa kuanza hivi karibuni katika Kata ya Bendera.
“Ukweli pasipo kupepesa macho na kwa moyo wa dhati kabisa nipende kuchukua nafasi hii kumpongeza ama niseme tuchukue nafasi hii kumpongeza Mama Anne Kilango nimfano wa kuigwa sana katika kuwatumikia wananchi hakika Mama ameheshimisha sana jimbo la Same mashariki kwani amekuwa na nia ya dhati kabisa kutetea haki na maslahi ya wananchi walio mchagua sisi kama madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Same tunampongeza sana na tunaahidi kuendelea kumpa ushirikiano “
“Alisema Mapande “.
Aidha Mapande amesema kamwe hawatasita kutoa pongezi kwa kiongozi yeyote ambaye atakuwa akifanya vizuri katika kuwatumikia wananchi.