Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan ametoa sababu za kumuondoa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata kwa kusema aliona mwisho wa siku ‘atadata’ (atachanganyikiwa).
Samia amesema “Kidata alifanya kazi nzuri lakini niliona atadata, sasa nakupeleka wewe kijana wa Dar es Salaam mtoto wa mjini uhuni wote uliopo TRA umeufanya na wewe humo humo pengine ulishiriki mipango yote ya kupenyeza unaijua Yussuph”
Rais Samia amesema hayo leo Julai 5, 2024 alipokuwa akiwaapisha viongozi mbalimbali walioteuliwa hivi karibuni, Ikulu ndogo Zanzibar.
Hivi karibuni Rais alimteua aliyekuwa Kidata kuwa Mshauri wa Rais, Ikulu nafasi iliyomuondoa katika nafasi yake ya awali.
Kidata ameondolewa TRA ikiwa ni wiki moja ipite tangu mgomo wa wafanyabiashara Tanzania ufanyike wakilalamikia utitiri wa kodi unaotozwa na TRA.