Serikali ya Tanzania kuendelea kushirikiana na wadau wa Maendeleo

Serikali ya Tanzania imebainisha kuwa imejidhatiti kuendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kuwawezesha vijana kupitia programu mbalimbali zinazotekelezwa nchini.

Inaelezwa kuwa hali hiyo itsaidia kuongeza ushiriki wa vijana katika maendeleo endelevu ya taifa.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa mradi wa BBT, Vumilia Zikankuba wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kongamano la vijana wanaofanya shughuli za kilimo nchini linalotarajiwa kufanyika Julai 5 mwaka huu.

Katika mkutano huo mbele ya waandishi wa Habari, Zikankuba alisisitiza kuwa miradi hiyo inawagusa vijana Wakitanzania bila kujali tofauti za elimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa shirika la AGRA Vianey Rweyendela amesema kongamano hilo limelenga kuongeza ushiriki wa vijana katika kilimo kwa kutambua mahitaji yao na hivyo kutanua wigo wa ajira nchini.

Related Posts