SINGIDA Fountain Gate imeonyesha nia ya kumpa mkataba mpya nyota wa timu hiyo Mghana Nicholas Gyan kwa ajili ya msimu ujao.
Nyota huyo wa zamani wa Simba aliyefunga mabao manne katika Ligi Kuu Bara msimu uliopita, mkataba alionao na Fountain umeisha rasmi, ingawa inaelezwa Gyan atakubali kusaini kuendelea kuichezea timu hiyo kwa msimu ujao ikiwa atalipwa fedha zake zote anazowadai.
Gyan anasifika kwa kumudu kucheza zaidi ya nafasi moja uwanjani aliwahi kuiburuza klabu hiyo katika Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) wakati huo ikifahamika kama Singida Fountain Gate kutokana na madai hayo ya fedha.