SERIKALI imewaagiza walimu wakuu wa shule za msingi nchini kuhakikisha wanaweka mifumo na mikakati thabiti ya kuwalinda Watoto dhidi ya unyanyasaji na ukatili wa aina yoyote ili kufanya shule kuwa mazingira salama kwao.
Hayo yamesema na Katibu Mkuu wa wizara ya Elimu sayansi na Teknoljia Profesa Carolyne Nombo katika hotuba yake iliyosomwa na Kamishna wa elimu kutoka wizara ya elimu Dk. Lyambwene Mutahabwa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa walimu wakuu na maafisa wa mazingira kuhusu ujenzi wwa miundombinu ya shule kupitia Programu ya BOOST na yanayofanyika mkoani Morogoro.
Dokta Mutahabwa amesema ujifunzaji bora unategemea uwepo wa mazingira salama na rafiki ya kujifunzia na kwamba uwepo wa vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi yao unapaswa kupingwa.
Hivyo anewaagiza walimu wakuu kuhakikisha wanaweka utaratibu wa kuwa na vilabu vya wanafunzi sambamba na kuwajengea uwezo wanafunzi kujitambua, kujieleza na kujiamini ili waweze kueleza changamoto zao na ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Aidha ameashauri walimu hao kuishirikisha jamii na kuweka utaratibu wa kubaini na kushughulikia masuala ya ukatili, unyanyasaji na malalamiko yanayojitokeza ikiwemo kuyafikisha kwenye mamlaka husika kwa yale yalito juu ya uwezo wa shule na kufanya ulinzi na usalama wa mtoto kuwa kipaumbele chao.
Akizungumzia program ya Boost anasema tayari serikali imejenga shule mpya za msingi 302 pamoja na miundombinu mingine ambapo jumla ya vyumba vya madarasa 7,230 na matundu ya vyoo 11,297 vimeshakamilika
Naye Mratibu Programu ya BOOST Ally Swalehe anasema maboresho mbalimbali ya mradi yameleta mafanikio makubwa ikiwemo ongezeko la uandikisha wanafunzi katika elimu ya awali na msingi na ongezeko la kiwango ujifunzaji wa mwanafunzi katika shule zote nchini.
Anasema program hiyo pia inakabiliwa na changamoto ongezeko la uhitaji wa miundombinu ya shule na ujifunzaji kwa maana ya ubora wa timu nzima ya kufundisha na kujifunza ambapo zipo baadhi ya shule zina wanafunzi ambao hawawezi kujimudu katika stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) hivyo progamu hiyo imeanzishwa na kuwa mtetezi kwao.
Naye Mshiriki Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Pangani mkoani Tanga Daudi Mlahagwa anasema mafunzo hayo yatawasaidia katika kutekeleza miradi inayogusa jamii ili kupiga hatua katika maendeleo.
Naye Mkuu wa shule ye Msingi Mzalendo iliyopo Manispaa Moshi Pascal Shirima aliishukuru serkali kwa kuwapatika mafunzoambayo anamini yatawasaidia katika kuwaongezea uzoefu katika masuala ya miradi na kuondoa dosari ndongondogo wanazokumbana nazo wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.