Watuhumiwa walioteka 100 hawajafikishwa mahakamani, THRDC wataka tume huru

Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa wito kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuunda tume huru ya kuchunguza matukio yote ya utekaji kuanzia mwaka 2016 hadi sasa hasa ikizingatiwa hata katika matukio makubwa ya utekaji hakuna watuhumiwa waliokamatwa na kufikishwa mahakamani. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Amesema hatua hiyo itasaidia kuchunguza matukio ambayo vyombo vya dola hususani Jeshi la Polisi vinavyotuhumiwa kwa utekaji mathalani tukio Ediger Mwakabela (Sativa) ambaye alitekwa hivi karibuni kisha Rais Samia kutangaza kugharamia matibabu yake.

Roma Mkatoliki

Wito huo umetolewa leo Ijumaa na Mkurugenzi wa mtandao huo, Onesmo Olengurumwa wakati akiwasilisha ripoti ya hali ya watetezi wa haki za binadamu na nafasi za kiraia.

Ametoa mfano matukio makubwa kama ya utekaji wa mfanyabiashara maarufu Mohamed Dewji “Mo Dewji”, msanii Roma Mkatoliki hadi sasa haluna watuhumiwa waliokamatwa.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2019 karibu watu 100 walitekwa lakini hakuna mtuhumiwa hata mmoja aliyefikishwa mahakamani.

Akizungumzia hali ya utekaji, Olengurumwa ameelezwa kushangazwa na kauli ya hivi karibuni kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni kuwa watuhumiwa wa matukio mengi ya utekaji wamefikishwa mahakamani.

Masauni alidai katika kipindi cha kuanzia Januari mwaka huu hadi Juni, kumetokea matukio nane ya utekaji huku asilimia kubwa ya watuhumiwa wakifishwa mahakamani.

Aidha, Olengurumwa amesema inadhihirisha kuwa matukio hayo yanahusu raia kwa raia kutekana kwa malengo ya kujipatia fedha, lakini matukio ya raia kudaiwa kutekwa na vyombo vya dola hakuna watuhumiwa waliofikishwa mahakamani hadi sasa.

“Kama polisi anatuhumiwa hawezi kujichunguza, wenzetu Afrika kusini wa mifumo dhabiti ya kuchunguza vyombo vya dola.  Leo unapeleka wapi taarifa za Sativa kwa waliodaiwa kumteka. Lazima kuwe na taasisi za kudumu kuhakikisha matukio yote ya utekaji yanafanyiwa kazi,” amesema.

Related Posts