Zuhura Yunus ahimiza watumishi kutatua changamoto za wananchi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Zuhura Yunus amewahimiza watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kutatua changamoto za wananchi na kuwaelimisha kuhusu masuala mbalimbali yanayotekelezwa.

Zuhura ameyasema hayo leo Julai 5,2024 alipotembelea banda jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba.

Katika maonesho hayo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Naibu Katibu Mkuu huyo ametembelea idara, vitengo na taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kujionea namna huduma zinavyotolewa kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo.

Related Posts