JAJI MKUU WA TANZANIA ATEMBELEA BANDA LA TUME YA USHINDANI (FCC) NA KUIPONGEZA KWA KAZI NZURI

Na Mwandishi Wetu

JAJI Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamis Juma amesema uwepo wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) na utekelezaji wa sheria ya ushindani vinalenga kuzuia athari za ukiritimba katika soko pamoja na kuondoa vizuizi vya uwekezaji katika maeneo mbalimbali.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma alipotembelea banda la FCC katika maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba mesisitiza kuwa sheria ya ushindani ni msingi wa ustawi na uchumi katika nchi zilizoendelea.

Prof. Ibrahim amesema kuwa licha ya FCC kuzuia athari za ukiritimba katika soko pia hurekebisha na kuwachukulia hatua wale wote wanaokikuka Sheria ya Ushindani, pamoja na kufanya biashara ya bidhaa bandia.

“Nawapongeza sana FCC kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kusimamia ushindani wa kibiashara unaopelekea kuvutia uwekezaji nchini.”amesema Prof. Ibrahim.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma (FCC) Bi. Roberta Feruzi alipotembelea banda hilo wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba Jijini Dar es Salaam.


Maofisa wa FCC wakitoa elimu kwa wanachi waliotembelea banda la FCC wakati wa maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Related Posts