SAA chache baada ya timu ya taifa, Taifa Stars kupangwa kundi moja na DR Congo, Guinea na Ethiopia katika kuwania kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 zitakazofanyikia Morocco, kocha mkuu wa timu hiyo, Hemed Suleiman ‘Morocco’ amekiri hilo sio kundi jepesi na kwamba Tanzania ni lazima ikaze kwelikweli ili iende fainali za nne za Afcon.