Wasanii wa Tanzania wakutana na star mkubwa sana wa Korean drama, Son Ye-jin.

Balozi wa Tanzania Korea, Mh. Togolani Edriss Mavura ameambatana na wasanii aliowaalika kufanya ziara Korea kusini kwaajili ya kuimarisha mahusiano na kubadilishana ujuzi katika soko la filamu. Wasanii walikutana na Son Ye-jin kubadilishana mawazo na kisha kukaa na watengeneza filamu wakubwa Cheol-ha Lee na Yohwan KIM.

Director Cheol-ha Lee amesema yupo katika maandalizi ya filamu itakayohusisha waigizaji international na angependa kupata muigizaji kutoka Tanzania kwa Afrika. Katika kikao hicho walitoa mawazo mbalimbali ikiwemo serikali kuweka nguvu katika kuinua wasanii wadogo kwa makusudi kabisa.

Wamepokea mualiko kutoka kwa rais Samia Suluhu Hassan, kuja Tanzania kuchagua maeneo mbalimbali ya kufanyia filamu zao na kisha kutembelea vivutio vyetu. Wameshukuru sana kwa zawadi za shuka za kimasai walizovalishwa na kiongozi wa msafara Steve nyerere, msanii Irene Uwoya na Blandina Chagula (Johari).

.
.
.
.
.
.
.
.

 

.
.
.
.
.
.
.
.

Related Posts