Mwalimu wa Urembo Chuo VETA Shinyanga Judi Mwita akionesha umahiri wa kunyoa kwenye Banda la VETA.
*Kusema kazi za wanaume ni ndio kufanya kuwepo kwa mfumo dume.
Na Mwandishi Wetu
MWALIMU wa Urembo wa Chuo cha VETA Shinyanga Judi Mwita amesema kuwa wasichana wajifunze masuala ya Urembo ikiwemo unyoaji nywele za kiume kutokana na kuwepo kwa soko kubwa ya wahitaji wa huduma hiyo.
Mwita ameyasema hayo katika Banda la VETA katika Maonesho ya 48 Biashara Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.amesema hata yeye hakuamini kama anaweza kunyoa aina tofauti ya nywele za kiume lakini ameweza na kuwa Mwalimu baaada kusoma taaluma mafunzo ya Ufundi Stadi.
Judi amesema kuwa kitendo cha wanawake kubagua kazi kwa kusema wanaweza wanaume kunawapotezea fursa nyingi za kujiendeleza kiuchumi.
“Hatuwezi kuacha kufanya kazi katika vizingizio vya kuwa kazi zingine wanaweza wanaume hapana tunatakiwa wanawake tujitume na hiyo ndio inaondoa mfumo dume” amesema Judi
Hata hivyo amesema kuwa katika kipindi cha sasa Teknolojia imekuwa kubwa vitu vingi vimerahisishwa na kufanya kutokuwa changamoto ya wanawake kutofanya.
Judi amesema kuwa kazi ya Urembo inalipa kwani watu wanataka kupendeza wakati wote hivyo mtu akipata mafunzo ajira yake iko mikononi mwake.