Mchezo wa soka watumika kuhamasisha vijana kujitokeza na kushiriki kwenye uchaguzi

Ili kufikia malengo ya uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Mwezi October mwaka huu 2024,wadau wa michezo mkoani Njombe wameanza kutumia michezo ikiwemo mpira wa miguu kuhamasisha wananchi hususani vijana kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kushiriki uchaguzi.

Mpete Diwani Cup ni moja ya ligi iliyozinduliwa mkoani Njombe ambapo mashindano haya yanasimamiwa na mwenyekiti wa hamshauri ya mji wa Njombe ambaye ni diwani wa kata ya Utalingolo Erasto Mpete,anasema dhamira kubwa ya mashindano hayo ni kuhamasisha vijana kuelekea kwenye uchaguzi na kuchagua viongozi bora.

“Ligi yetu inahamasisha vijana kwa wazee kuhakikisha wanajitokeza kwanza kijiandikisha kwenye daftari la wapiga kura lakini pili kujitokeza mwezi wa kumi kuchagua viongozi walio bora”amesema Mpete

Kwa upande wake Erasto Ngole aliyewahi kuwa katibu wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Njombe ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Shikamoo Parachichi ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano hiyo ametoa wito kuwachagua wanaofaa kwa ajili ya maendeleo.

“Kama kuna mtu mnaona anafaa kuwa kiongozi naa anaweza kuungwa mkono na wananchi ilimradi anatoka ndani ya CCM nendeni mkamshawishi agombee bila kuwasahau akina mama”amesema Ngole

Kwa upande wao vijana wanaoshiriki kwenye michezo akiwemo Osward Mligo na Festo Mligo wanasema kupitia mashindano hayo zipo faida nyingi wanazozipata ikiwemo kuboresha afya zao huku wakipongeza kubeba ujumbe wa kuhamasisha maswala ya uchaguzi.

Related Posts