Rwanda wanashirikiana na waasi M23 dhidi ya DRC

Ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa imesema karibia wanajeshi wa Rwanda karibu 3,000 hadi 4,000 wanapigana pamoja na waasi wa M23 nchini DRC. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ambayo imeonekana na shirika la habari la AFP, Kigali inaongoza harakati za waasi hao wa M23.

Mkoa wa Kivu Kaskazini nchini DRC umekuwa ikishuhudia uasi wa wapiganaji wa M23 tangu mwishoni mwa mwaka wa 2011 ambapo wameelezwa kuchukua baadhi ya miji kwenye eneo hilo.

Kinshasa inaituhumu Rwanda kwa kuwaunga mkono na kuwafadhili waasi hao, madai ambayo Kigali kwa upande wake imeendelea kukanusha.

Licha ya Rwanda kukana madai ya Kinshasa, Ripoti ya iliyozinduliwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa imeeleza kwamba hatua ya Kigali kuwaunga mkono waasi hao ina maana kwamba inawajibikia vitendo vinavyotekelezwa na M23.

Rais wa Rwanda Paul Kagame

Ripoti hiyo imeeleza kwamba wanajeshi wa Rwanda (RDF) kupitia oparesheni zao katika maeneo ya Nyiragongo, Rutshuru na Masisi katika jimbo la Kivu Kaskazini ziliwasaidia wapiganaji wa M23 kuchukua maeneo zaidi kati ya mwezi Januari hadi mwezi Machi mwaka huu.

Wataalam hao vilevile wamesema kwamba wakati wakiandika ripoti hii mwezi Aprili, idadi ya wanajeshi wa Rwanda ilikuwa inalingana au kuzidi ile ya waasi wa M23 wanaoaminika kuwa 3,000

Ripoti hiyo ina picha, video zilizonaswa na ndege zisizo na rubani, rekodi za video, ushuhuda na intelenjisia inayothibitisha matukio ya wanajeshi wa Rwanda kuvuka mpaka.

Video na picha pia zinawaonyesha watu wenye silaha wakiwa na mavazi rasmi wakiwa na magari ya kivita, vifaa vya kuzuia makombora sawa na malori ya kuwabeba wanajeshi.

Aidha, ripoti hiyo pia inayoosha kuwa watoto kuanzia miaka 12 wamesajiliwa kutoka karibia kambi zote za wakimbizi nchini Rwanda ambao wanatarajiwa kutumwa katika kambi za mafunzo katika maeneo yanayokaliwa na waasi chini ya uongozi wa wanajeshi wa Rwanda na waasi wa M23.

Related Posts