Dar es Salaam. Miongoni mwa wamachinga wakieleza sababu ya kumkataa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Hassan Bomboko na kufanya mgomo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.
Miongoni mwa sababu hizo ni kile walichodai hawana imani naye katika kushughulikia changamoto zao.
Mzizi wa maandamano na mgomo wa wafanyabiashara katika soko hilo ni uamuzi wa Manispaa ya Ubungo kutangaza kulikabidhi eneo hilo kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart).
Manispaa hiyo imetoa tangazo hilo, Julai 4, 2024 baada ya kikao cha Baraza la Madiwani.
Endelea kufuatilia Mwananchi