Dar es Salaam. Siku mbili baada ya Gazeti la Mwananchi kuripoti uwepo wa madaktari 3,000, wauguzi 25,000 nchini kukosa ajira, Serikali imetangaza nafasi 9,483 mpya za ajira katika sekta hiyo.
Tangazo hilo la nafasi za ajira limetolewa jana Jumapili Julai 7, 2024 na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa.
“Sekretarieti ya ajira inakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 9,483 kama ilivyoainishwa katika tangazo hili,” imeeleza taarifa hiyo.
1. Fundi sanifu vifaa tiba daraja la II (Biomedical engineeringe technician II) nafasi 86
2. Tabibu msaidizi daraja la II (Clinical assistant II) – nafasi 636
3. Ofisa mlezi wa watoto msaidizi daraja la II (Assistant child care officer grade II) – nafasi 2
4. Ofisa muuguzi daraja la II (Nursing officer II) – nafasi 301
5. Ofisa muuguzi msaidizi daraja la II – (Assistant nursing officer II) nafasi 1,016
6.0 Tabibu daraja la II (clinical officer II) nafasi – 1,239
7. Mfamasia daraja la II (Pharmacist II) nafasi – 128
8. Dobi (Launderer) – nafasi 5
9. Ofisa mteknolojia daraja la II – maabara (Health laboratory scientists II) – nafasi 57
10. Fiziotherapia daraja la II (physiotherapist II) – nafasi 83
11. Daktari bingwa wa kinywa na meno daraja la II (dental secialist)
12. Daktari wa upasuaji wa kinywa na meno daraja la II (Dental surgeon ii) – nafasi 111
13. Tabibu wa kinywa na meno daraja la II (Dental therapist ii) – nafasi 210
14. Katibu wa afya daraja la II (Health secretary ii) – nafasi 41
15. Ofisa fiziotherapia dalaja la II (Physiotherapy officer ii) -nafasi 11
16. Ofisa afya mazingira daraja la II (Enviromental health officer ii) – nafasi 124
17. Ofsa afya mazingira msaidizi daraja la II (Assistant enviromental health officer ii) – nafasi 276
18. Msaidizi afya ya mazingira daraja la II (Enviromental health assistant ii) – nafasi 122
19. Mteknologia msaidizi daraja la II – maabara (Assistant laboratory technologist ii) – nafasi 146
20. Mteknolojia msaidizi – radiolojia (Assistant technologist -radiology ii) – nafasi 15
22. Ofisa lishe daraja la II (Nutrition officer ii) – nafasi 129
23. Fundi sanifu msaidizi vifaa tiba (Assistant biomedical technician) – nafasi 5
24. Daktari bingwa wa watoto daraja la II (Medical specialist – peditrician ii) – nafasi 4
25. Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani daraja la II (Medicale specialist – internal medicine ii) – nafasi 7
26. Daktari bingwa wa magonjwa ya wakina mama daraja la II (Medical specialist – gynaecologist ii) – nafasi 9
27. Daktari bingwa wa upasuaji daraja la II (Medical specialist – general surgeon ii) – nafasi 5
28. Daktari bingwa wa masikio, pua na koo daraja la II (Medical specialist – ear, nose and throat II) – nafasi 1 Dar es Salaam
29. Daktari daraja la II (Medical officer II) nafasi – 726
30. Mhandisi vifaa tiba daraja la II (Biomedical engineer II)
31. Msaidizi wa afya (Health assistant) nafasi – 1,057
32. Mtoa tiba kwa vitendo daraja la II (Occupational therapist II) – nafasi 12
33. Mteknolojia wa maabara daraja II (Health laboratory technologist II) – nafasi 322
34. Mteknolojia wa radiografa daraja II – radiolojia (Radiography technologist II – radiology) – nafasi 103
35. Mteknolojia dawa daraja II – (Technologist pharmacy II) nafasi 128
36. Mteknolojia wa macho daraja II (Technologist – optometrist II) nafasi 6
37. Mteknolojia wa meno daraja II (Dental technologist II) nafasi 3
38. Muuguzi II (nurse II) – nafasi 2,282
Taarifa hiyo imewataka waombaji waliostaafishwa katika utumishi wa umma kuwa hawaruhusiwi kuomba, isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
“Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010,” imeeleza taarifa hiyo.
Pia imesisitiza wawasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi, wahusika watachukuliwa hatua za kisheria na kwamba mwisho wa kutuma maombi hayo ya kazi ni Julai 20, 2024.