Tume ya Ushindani (FCC), imeendelea kutumia fursa ya Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) kwa kutoa elimu kwa Umma ambao ndio walaji au watumiaji wa bidhaa na huduma.
Wananchi mbalimbali wameendelea kujitokeza na kutembelea banda la FCC ambapo wamenufaika kwa kupata elimu zaidi inayohusu masuala ya Ushindani, Udhibiti wa Bidhaa Bandia na Kumlinda Mlaji kutoka kwa wafanyakazi wa FCC.
Maonesho haya yaliyoanza tarehe 28 Juni na kufunguliwa rasmi tarehe 3 Julai, 2024 yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 13 Julai, 2024.