Uzinduzi wa wiki ya wazazi kitaifa Katavi

Makamu wa Pili wa Rais, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman Abdullah amemwakilisha Rais wa SMZ, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi katika uzinduzi wa Wiki ya Wazazi Kitaifa leo Julai 8, 2024 katika viwanja vya Shule ya msingi Inyonga, Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar akiwemo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) kutokea jumuiya ya Wazazi pamoja na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Ushindi wa CCM 2024 – 2025”.

Related Posts