Waziri mkuu akuta madudu bwalo la milioni 774

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambana Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo kushindwa kusimamia matumizi ya Fedha ujenzi wa Bwalo shule ya Sekondari ya Wasichana Lugalo ambayo ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa shule hiyo

Ashangazwa kutumika kwa fedha yote ya ujenzi wa Bwalo lakini mpaka sasa halijakamilika.

Bwalo hilo lilipangiwa sh. milioni 774 na wamekwishatumia sh. milioni 341 hadi kufikia hatua ya linta ambayo ni sawa na asilimia 40 ya ujenzi wake.

Aagiza asimamishwe kazi kupisha uchunguzi, yumo pia Mkurugenzi Mstaafu wa Halmashauri aliyestaafu mwezi Aprili mwaka huu, ambapo Majaliwa aagiza aitwe na ahojiwe.

Related Posts