Ant Man amzingua LeBron | Mwanaspoti

SUPASTAA wa Ligi ya Kikapu Marekani (NBA), Anthony Edwards ‘Ant Man’ ametoa kali ya kushtua kuelekea michuano ya Olimpiki nchini Ufaransa mwishoni mwa mwezi huu, akidai ndiye nyota wa kutumainiwa kwa timu ya Taifa ya mchezo huo huko Marekani kwenye michuano hiyo.

Ant Man alikuwa na msimu bora sana uliopita akiwa na Minnesota Timberwolves iliyoishia nusu fainali ya Ukanda wa Magharibi mbele ya Dallas Mavericks baada ya kuivua ubingwa Denver Nuggets.

Alipoulizwa juu ya uwepo wa mastaa wakubwa walio na kila sifa za ubora kwa muda mrefu kumzidi, LeBron James, Steph Curry, Kevin Durant, Kawhi Leonard na Anthony Davis, nyota alizingua akisisitiza wanatakiwa kumtegemea na kuamini ataibeba timu nzima kufanya vyema kwa kuchukua taji la Olimpiki. Nyota huyo alisema kwenye Olimpiki ijayo anaamini ataendeleza moto aliokuwa nao NBA, kiasi kwamba timu nzima inatakiwa imzunguke e kuwa kama mchezaji wa kuiongoza Marekani kubeba taji hilo mwaka huu.

Related Posts