Balozi Said Mussa anena ‘Somo la Dkt Samia limeeleweka vyema na linatekelezwa kwa vitendo’

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaibu Mussa ameipongeza Benki ya CRDB kwa uamuzi wenu wa kufanya CRDB Bank Marathon katika nchi tatu kwa maana ya Tanzania, Burundi na DRC.

Balozi Mussa amesema uamuzi huo unaenda sambamba na jititihda zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuifungua nchi na kuboresha mahusiano ya kidiplomasia na jirani zetu.

“Hivyo tunapoona taasisi binafsi kama Benki ya CRDB mkipita katika njia hizo hizo kwa kutoishia kukuza biashara zenu nje ya mipaka bali kuangalia namna gani mnaweza kugusa maisha ya watu katika nchi hizo, tunapata faraja na kuona somo la Dkt. Samia limeeleweka vyema na linatekelezwa kwa vitendo. Hongereni sana,” awesema Balozi Mussa.

.

Related Posts