CHAGUENI VIONGOZI WATAKAOSHIRIKIANA NA MHE. RAIS KUTATUA KERO – MHE. KATIMBA 

Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba amewataka wananchi kuchagua viongozi bora katika uchaguzi ujao wa Serikali za Mitaa ambao watamuunga mkono kwa vitendo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kutatua kero na changamoto zinazowakabili.

Mhe. Katimba ametoa wito huo kwa watanzania wote, akiwa wilayani Uvinza, mara baada ya kutakiwa na Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango kuzungumzia umuhimu wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024.

Mhe. Katimba amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kujiandikisha kwenye daftali la mkazi ili kupata nafasi ya kupiga kura na kuchagua viongozi wenye sifa ya kulitumikia taifa.

“Usipojiandikisha kwenye daftari la mkazi ni wazi kuwa, utakosa haki yako ya msingi ya kupiga kura ili kuchagua viongozi wenye sifa stahiki ya kuitumikia jamii kupitia Serikali za Mitaa,” Mhe. Katimba amesisitiza.

Mhe. Katimba amewahimiza wananchi katika maeneo yao, kuchagua viongozi bora wanaochapa kazi, wanaowajibika na waadilifu na sio wale wanaotoa rushwa ili wachaguliwe.

Sanjari na hilo, Mhe. Katimba amewaka wanawake nchini kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili washiriki kikamilifu katika kutatua kero na changamoto zinazowakabili wananchi, ikiwa ni pamoja na kuliletea taifa maendeleo.

Related Posts