Hamilton mzuka tu langalanga | Mwanaspoti

HAIKUWA rahisi dereva Lewis Hamilton kuamini ameshinda mbio za magari duniani baada ya miaka miwili na nusu, tangu mara ya mwisho aliposhinda mwishoni mwa mwaka 2021.

Hamilton, bingwa mara Saba wa mbio za magari duniani (formula one) alimaliza ukame wa mbio 56 bila ushindi, akishinda za wikiendi iliyopita Uingereza na akiweka rekodi mpya ya kuwa dereva wa kwanza kushinda jumla ya mbio 104.

Ushindi huo wa mbio tisa pia za Uingereza pekee, ulikuwa wa pili mfululizo kwa Kampuni ya Mercedes kushinda baada ya dereva George Russell wa kampuni hiyo pia kushinda wiki moja nyuma Austria.

Hamilton anadai mbio hizo ndizo za kusisimua zaidi kwake tangu aanze kushinda mbio za magari kutokana na kumpa tumaini jipya la kufanya vyema katika mbio hizo alizokaribia kuachana nazo kutokana na kutoshinda muda mrefu.

Related Posts