Huu ndio msimu mpya wa CRDB Marathon, Mkurugenzi Mtendaji afunguka haya

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Group, Abdulmajid Nsekela ambaye ndiye Jenerali wa Jeshi la Kusambaza Tabasamu (JLKT) la CRDB Bank Marathon amekabidhi bendera maalum ya jeshi hili ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa msimu wa tano mbio hizo na kukabidhi mamlaka kwa Jeshi letu la JKLT kusambaza tabasamu Tanzania, Burundi na DRC.

Malengo msimu wa tano wa CRDB Bank Marathon ni kusajili wanajeshi wa kusambaza tabasamu (washiriki) zaidi ya 8,000 na kukusanya zaidi ya shilingi bilioni 2. Katika msimu huu, CRDB Bank Marathon inatarajia kuanzia jijini Lubumbashi nchini DRC Agosti 4 kisha tutaelekea jijini Bunjumbura nchini Burundi Agosti 11 kabla ya kurudi hapa Dar es Salaam Agosti 18.

.

Pamoja na makundi mengine ambayo yamekuwa yakinufaika na mbio hizo ikiwamo Watoto wenye maradhi ya moyo, na wakinamama wenye ujauzito hatarishi mwaka huu katika kuendeleza azma ya uwezeshaji kwa vijana sehemu ya fedha zitakazokusanywa zitakwenda kusaidia jitihada za kuwajengea uwezo vijana nchini (capacity building).

“CRDB tupo mpaka Burundi. Na kule kuna Matawi manne makubwa ya CRDB na kuna mawakala 1500”

“Kwa sasa CRDB inaongoza kwa faida nchini Burundi. Ukifika kule na ukatumia Benki ya CRDB hutaona tofauti na ukiwa Tanzania”

“Natoa shukrani kwa Serikali ya Burudi kwa sapoti kubwa hasa kutoka kwa Rais wa Burundi Mhe. Evarist Ndayishimiye” – Jenerali wa Jeshi La Kusambaza Tabasamu AbdulMajid Nsekela.

“Uwepo wenu wote hapa unamaanisha kwamba tabasamu limekuja na ndio maana mko hapa.
Benki ya CRDB ni Benki ya kizalendo, benki yenye maono na inayojitofautisha na wengine. Hii ndio tofauti ya CRDB na Benki nyingine.” – Jenerali wa Jeshi La Kusambaza Tabasamu Mhe. AbdulMajid Nsekela

.

Related Posts