MAANDALIZI YA MKUTANO WA 26 WA KAMATI YA MAWAZIRI WA ASASI YA SIASA, ULINZI NA USALAMA YA SADC YAANZA JIJINI LUSAKA

Mbali na Balozi Shelukindo, viongozi wengine kutoka Tanzania wanaoshiriki Mkutano wa Makatibu Wakuu ni pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda, Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Lt. Jen. Mathew Mkingule, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri na Maafisa Waandamizi wa Wizara na Vyombo vya ulinzi na Usalama.

Mwenyekiti wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambaye pia ni Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Zambia, Bi. Etambuyu Gundersen akifungua rasmi mkutano huo uliofanyika tarehe 8 Julai 2024 jijini Lusaka, Zambia. Mkutano huo ni maandalizi ya Mkutano wa 26 wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa SADC unaotarajiwa kufanyika tarehe 11 na 12 Julai 2024


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC unaofanyika jijini Lusaka, Zambia tarehe 8 na 9 Julai 2024

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe (kushoto) akiwa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Jacob Mkunda (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Kamishna wa Polisi Salum Hamduni (kulia) wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Lusaka, Zambia

Balozi Shelukindo akimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Talha Waziri wakati akifafanua jambo kwake kuhusu agenda za mkutano


Ujumbe wa Zambia ambao ni wenyeji wa Mkutano huo wakishiriki hafla ya ufunguzi


Ujumbe wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu

Ujumbe wa Madagascar wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu

Ujumbe wa Malawi wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu

Ujumbe wa Angola wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu

Ujumbe wa Lesotho wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu


Ujumbe wa Botswana wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu


Ujumbe wa Msumbiji wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu

Ujumbe wa Shelisheli wakishiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bibi. Talha Waziri akifuatilia hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kamati ya Makatibu Wakuu wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC

Mkutano ukiendelea

Related Posts