MAMLAKA YA DAWA NA VIFAA TIBA (TMDA), IMETOA WITO KWA WANANCHI KUENDELEA KUZINGATIA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA

 

 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Adam Fimbo, akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Maonesho  ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Na: Mwandishi wetu

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), imetoa wito kwa wananchi kuendelea kuzingatia matumizi sahihi ya Dawa na kuacha kutumia bidhaa hiyo kiholela bila kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu.

Kauli hiyo imetolewa na  Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Adam Fimbo kwenye Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba), yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Fimbo amesema kuwa Mamlaka hiyo inaendelea kupambana na usugu wa vimelea vya Dawa na kuelimisha jamii katika kuhakikisha Dawa zinatumika kwa ufasaha na usahihi kwakufuata maelekezo sahihi ya Kitaalam.

“Usugu wa Dawa umekuwa ukiongezeka siku hadi siku kutokana na matumizi ambayo sio sahihi, nakupelekea wananchi wengi kupata madhara” amesema.

Amesema TMDA imeshiriki maonesho ya Sabasaba mwaka huu ili kutoa elimu kwa wananchi juu ya matumizi sahihi ya Dawa na kufahamu majukumu ya Taasisi hiyo.

Aidha ametoa mwito kwa wananchi kuendelea kutembelea kwenye banda lao  kupata elimu ya udhibiti na matumizi sahihi ya Dawa awa na vitenganishi.

Related Posts