Nigeria. Nchi ya Nigeria inapanga kusitisha ushuru kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kutoka nje ikiwa ni pamoja na ngano na mahindi kwa siku 150, ili kujaribu kudhibiti kupanda kwa bei katika taifa hilo lenye watu wengi zaidi barani Afrika.
Reuters imemnukuu Waziri wa Kilimo wa Nigeria, Abubakar Kyari jana Jumatatu kwamba hatua hiyo ni sehemu ya sera ya Serikali ya kukabiliana na mfumuko wa bei za vyakula.
Mfumuko wa bei ambao umepanda hadi zaidi ya asilimia 40 mwaka hadi mwaka, na kuchochea ukuaji ambao umekuwa tete kwa takriban muongo mmoja.
Rais Bola Tinubu ameitaka timu yake ya usimamizi wa uchumi kuandaa mpango wa kichocheo wa Naira 2 trilioni (Dola bilioni 1.33) ili kushughulikia wasiwasi kuhusu usambazaji wa chakula na bei na kuimarisha sekta muhimu.
Hata hivyo waziri wa kilimo Kyari amesema ili kupunguza mfumuko wa bei za vyakula nchini humo unaosababishwa na uwezo wa kumudu bei na kuchochewa na upatikanaji, serikali imechukua hatua kadhaa kutekelezwa katika siku 180 zijazo.
Waziri huyo amesema serikali itaagiza tani 250,000 za ngano na tani 250,000 za mahindi kutoka nje zikiwa zimechakatwa nusu na zile zinazolengwa kwa wasindikaji wadogo na wasagishaji.
Aidha, mfumuko wa bei ya vyakula umeongezeka katika taifa hilo la Afrika Magharibi huku kukiwa na ukosefu wa usalama katika sehemu za kanda zinazozalisha chakula nchini humo na mtandao mbovu wa barabara unaounganisha mashamba na masoko.
Kupanda kwa gharama za vyakula vikuu kumeongeza gharama na shida ya maisha na kuongeza mfumuko wa bei nambari mbili ambao umekwama kwa karibu miaka 30 ya juu.
Kyari amesema msamaha huo wa ushuru utahusu bidhaa za chakula zinazoingizwa nchini kupitia mipaka ya nchi kavu na baharini.